Rais Ruto aelezea mikakati ya kuimarisha utalii Pwani

  • | K24 Video
    32 views

    Raisi William Ruto ameanza ziara yake ya wiki moja Pwani mwa Kenya hii leo huku akishuhudia kuwasili kwa meli ya watalii Norwegian Dawn iliobeba watalii 2200 ambao wamepata nafasi ya kuzuru vivutio mbalimbali vya utali nchini. Rais Ruto amekitaja kitengo cha utalii kupitia usafiri wa meli kama kinachoanza kuimarika huku taifa likisajili mapato ya shilingi bilioni 450 kutoka kwa sekta ya utalii mwaka uliopita.