Rais Ruto atoa hakikisho kuwa mahifu waliotekwa nyara na magaidi watarejeshwa nyumbani salama.

  • | K24 Video
    383 views

    Rais William Ruto ametoa hakikisho kuwa chifu watano waliotekwa nyara na magaidi Mandera watarejeshwa nyumbani salama. Akiahidi kupambana na makundi ya kigaidi, Ruto amemuagiza naibu inspekta jenerali Gilbert Masengeli kuhakikisha kuwa machifu hao wanapatikana. Akizuru maeneo ya kaskazini mashariki, Ruto ameshutumu siasa za kikabila huku akiwaahidi wakazi wa maeneo hayo kuwa watakuwa wakipokea vitambulisho bila ya kufanyiwa mahojiano.