Ruto na Wandani Wake Wazomewa Nyandarua

  • | K24 Video
    7,122 views

    Baada ya ziara yenye mafanikio ya siku mbili katika eneo la Mlima Kenya, Rais William Ruto na wandani wake walikumbana na upinzani mkali kutoka kwa wakazi wa Kaunti ya Nyandarua. Wabunge Mwangi Kiunjuri wa Laikipia Mashariki na Kimani Ichung’w’a wa Kikuyu walilazimika kukatiza hotuba zao baada ya kuzomewa na umati.Tukio hili linajiri siku moja tu baada ya Rais Ruto na washirika wake kumshambulia Naibu Rais Rigathi Gachagua katika mikutano ya hadhara Kirinyaga na Meru.