Baadhi ya maseneta wamemkosoa mmoja wao wanayedai anaunga mkono mateso ya wakenya katika mataifa jirani ya Uganda na Tanzania. Wakijadili hoja inayopendekeza uwekaji kamera za CCTV katika vituo vyote vya polisi, seli na eneo la utoaji ripoti kwa polisi, maseneta hao wakiongozwa na Enoch Wambua wa kaunti ya Kitui, walisema matamshi ya mwenzao wa Nandi Seneta Samson Cherargei ni ya kusikitisha yakijiri wakati ripoti zinaashiria kuwa takriban wakenya 20 walifariki katika vituo vya polisi mwaka huu pekee.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive