Wahudumu chini ya UHC wadai kupuuzwa na serikali

  • | KBC Video
    52 views

    Wahudumu wa afya chini ya mpango wa serikali wa afya kwa wote wanaishutumu serikali kwa kupuuza malalamishi yao licha ya kugoma kwa mwezi mmoja. Wahudumu hao walioandaa maandamano ya amani jijini Nairobi wameapa kutolegeza kamba na kuendelea kutetea maslahi yao hadi yatakaposhughulikiwa. Wahudumu hao wanataka kuajiriwa kwa masharti ya kudumu na kulipwa marupurupu ya baada ya mkataba pamoja na kuwasilishwa kwa matozo yao kwa hazina ya malipo ya kustaafu miongoni mwa malalamishi mengine.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive