Wasimamizi wakuu wa Adani washtakiwa Marekani

  • | Citizen TV
    3,012 views

    Hatua ya Rais William Ruto kufutilia mbali kandarasi iliyopewa kampuni ya adani ya kusambaza umeme na ukarabati wa uwanja wa jkia ulifuatia kushtakiwa kwa wasimamizi wakuu wa kampuni ya Adani nchini Marekani. Maafisa hao akiwemo mwenyekiti Gautam Adani walidaiwa kuahidi kutoa hongo ya zaidi ya shilingi bilioni 32 ili kupata zabuni ya kusambaza nguvu za umeme nchini India.