Watu 63 walazwa hospitali baada ya kunywa mursik

  • | Citizen TV
    1,955 views

    Watu zaidi ya thelathini wamelazwa hospitalini Londiani baada ya kunywa maziwa ya mursik yaliyoharibika siku ya Ijumaa. Watu hao ni miongoni mwa watu zaidi ya mia moja ambao walikunywa maziwa hayo katika hafla ya kufuzu kwa wanafunzi wa chuo cha Kericho school of preaching inadaiwa watu hao waliuziwa maziwa hayo ya mursik na mfanyibiashara mmoja ambaye anadaiwa kuwa mafichoni kwa sasa. Waliougua ni wanakijiji wa kabianga na masaita kaunti ya Bomet. Watu 12 ni miongoni mwa watu waliougua na wanapokea matibabu. Wagonjwa hao wanadaiwa kuharisha na kutapika.