Lissu aeleza uhusiano imara uliopo kati yake na Freeman Mbowe

  • | VOA Swahili
    835 views
    Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanya uchaguzi mkuu wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, uchaguzi uliyowakutanisha wagombea watatu wakuu: Tundu Lissu, Freeman Mbowe, na Odero Odero. Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa hatua muhimu katika mustakabali wa chama hicho, huku wagombea wakitoa wito wa mshikamano, maridhiano, na umoja ndani ya chama kwa ajili ya kuimarisha demokrasia na maendeleo nchini. Huu ulikuwa ujumbe maalum kutoka kwa mwanasiasa mkongwe Lissu kwa wajumbe na wanachama wa mkutano huo. Ripoti ya mwandishi wa VOA, Amri Ramadhani. #uchaguzi #chadema #mwenyekiti #makamu #tundulissu #freemanmbowe #voa #voaswahili