Watu 51 wauawa Ituri, DRC

  • | BBC Swahili
    1,989 views
    Watu 51 wameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka katika vijiji vya eneo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Inadaiwa kuwa vikosi vya CODECO vilishambulia vijiji vya Djaiba na kuteketeza nyumba zao, kuwakata kwa mapanga na kuwapiga risasi raia usiku wa jana. Kundi hilo pia linadaiwa kutekeleza mashambulizi katika kambi ya wakimbizi wa ndani kabla ya kutimuliwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa, MONUSCO.