Makubaliano ya Waasi wa Rapid Support Forces Yazua Wasiwasi wa Kidiplomasia Kati ya Kenya na Sudan

  • | K24 Video
    134 views

    Kundi la waasi wa Rapid Support Forces pamoja na makundi tofauti kutoka Sudan yametia saini makubaliano ya kubuni serikali mbadala nchini Sudan. Haya yanajiri licha ya wadadisi kuhoji kuwa hatua hiyo huenda ukapeleka uhusiano baina ya kenya na sudan kudorora zaidi, serikali ya kenya ikikashifiwa vikali kwa kukubali mazungumzo ya kundi hilo la waasi kufanya mkutano na kutia saini mkataba wao hapa nchini.