Upinzani Tanzania yadai Tundu Lissu amehamishwa

  • | BBC Swahili
    28,608 views
    Chama cha upinzani nchini Tanzania - CHADEMA, kimetoa taarifa inayodai kwamba mwenyekiti wake Tundu Lissu ambaye amekuwa akizuiliwa katika gereza la Keko jijini Dar es Salaam amehamishwa na hadi kufikia sasa hajulikani alipo. Kwa mujibu wa chama hicho, kiongozi huyo aliondolewa katika gereza hilo kwa msafara wa magari na kabla ya hapo, mawakili na familia hawakukubaliwa kumuona.