Rais William Ruto ametangaza kutolewa kwa kima cha dola za kimarekani bilioni 100 na taasisi za kifedha barani Afrika ili kuimarisha mbinu za kuhifadhi mazingira. Mkataba huo, ulioafikiwa katika kongamano kuhusu hali ya hewa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia linazileta pamoja taasisi kuu za kifedha barani humu kwa kile kinachosemekana kuwa mkataba mkubwa zaidi wa kifedha kuhusu hali ya hewa kuwahi kutiwa sahihi katika historia ya bara hili. Akizungumza wakati alipoongoza hafla ya kutiwa saini kwa mkataba huo, Rais Ruto alisema mkataba huo sio tu njia ya kupiga jeki kifedha miundomsingi bali pia unatoa nafasi za ajira kwa vijana wa bara hili, kugeuza rasilimali za kiasili pamoja na uwezo wa binadamu wa kuukweza uvumbuzi. Ben Chumba na taarifa kwa kina.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive