Baadhi ya shule zimeanza kuwatuma nyumbani wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu.

  • | Citizen TV
    2,140 views

    Huku mgomo wa walimu wa muungano wa KUPPET ukiingia wiki ya pili, katika kaunti ya Nakuru baadhi ya shule zimeanza kuwatuma nyumbani wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu. Tayari Wanafunzi wa shule ya Upili ya Jomo Kenyatta huko Nakuru wameanza kurudi nyumbani. Wazazi walipokea ujumbe na kutakiwa kufika shuleni kuwachukua watoto wao leo asubuhi. Tunaungana naye Evans Asiba kutoka kaunti ya Nakuru kwa maelezo zaidi.