Biashara kati ya Rwanda na DRC imeathiriwa vipi na waasi wa M23?

  • | BBC Swahili
    2,539 views
    Wafanyabiashara mjini Rubavu, magharibi mwa Rwanda, wanaovuka mpaka kati ya Rubavu na mji wa Goma ulio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanasema kuwa bidhaa wanazopeleka DRC zimepungua kwa kiasi kikubwa. Ni miezi miwili sasa tangu waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma. Licha ya uhuru uliopo sasa wa kusafiri na kufanya biashara kati ya wakazi wa miji hiyo, wafanyabiashara upande wa Rwanda wanalalamikia ukosefu wa pesa mjini Goma ambako hakuna benki inayofanyakazi.