Daktari

  • | VOA Swahili
    42 views
    Daktari wa Kipalestina Khaled al-Saedni anafanya kazi katika kitengo cha watoto cha hospitali ya Al-Aqsa Martyrs huko Gaza City. Daktari huyu, ambaye amefanya kazi katika hospitali hii kwa zaidi ya miaka 23, alipoteza mguu wake mwaka jana baada ya kujeruhiwa. Anasema alijeruhiwa na bomu katika kambi ya wakimbizi ya Al-Bureij katika miezi ya kwanza ya vita vya Gaza. Kutokana na matatizo yaliyotokana na maradhi ya kisukari, daktari huyu mwenye umri wa miaka 50 anasema, mguu wake ulikatwa. Lakini licha ya kutegemea kifaa cha kutembelea, daktari huyu wa watoto alisema amerejea kufanya kazi kuwahudumia watoto “katika fursa ya kwanza” aliyopata baada ya miezi kadhaa ya kufanyiwa upasuaji na kupata matibabu. “Nimepoteza mguu, namshukuru Mungu. Kuna watu familia zao nzima wamekufa shahidi – wake, watoto, wazazi na ndugu zao,” Saedni alisema, ana matumaini vita vya Gaza vitamalizika haraka. Israel ilianza mashambulizi ya angani na ardhini dhidi ya Gaza baada ya wapiganaji walioongozwa na Hamas kushambulia jamii za Waisraeli Oktoba 2023, na kuua watu 1,200 na kuwachukua mateka 250 kurejea nao Gaza, kulingana na hesabu za Isreali. Kampeni ya kivita ya Israeli tangu wakati huo imewauwa zaidi ya Wapalestina 46,500 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100,000, kulingana na wizara ya afya ya Gaza. Kampeni hiyo imewakosesha makazi watu milioni 2.3 na kuharibu eneo lote finyu la pwani. #ukandawagaza #daktari #khaledalsaedni #israel #mabomu #hamas #mateka #voa #voaswahili #kilema