Familia moja kaunti ya Narok inalilia haki baada msichana wao kuuawa na aliyekuwa mumewe

  • | Citizen TV
    1,534 views

    Familia moja kaunti ya Narok inalilia haki baada ya mpendwa wao kudaiwa kushambuliwa kwa panga na kuuwawa na aliyekuwa mumewe. inadaiw akuwa Martha Njeri aliyekuwa na umri wa miaka 22 alikuwa ametorokea kwa dadake katika kijiji cha Enabelbel Narok Kaskazini kufuatia mizozo ya ndoa ya kila mara ila mumewe alifuata hadi alikotorokea na kumshambulia. inadaiwa kuwa mshukiwa huyo, Peter Lemaiyan, aliyetoweka na kumwacha Njeri na majeraha ya panga . alifariki hospitalini baada ya kuvuja damu nyingi. Mshukiwa anadaiwa kuwatisha dada hao wawili wiki tatu zilizopita kwa kisu na alikuwa ameachiliwa kwa bondi ya polisi baada ya kukamatwa.