Wiki moja baada ya moto mkubwa kuzuka California na kusambaa bila kudhibitiwa, watabiri wa hali ya hewa wanabashiri kwamba upepo mkali na hatari unaojulikana kama santa Ana unaweza kutokea.
Baadhi ya maeneo ya Los Angeles na mengine Jirani ya jimbo la Ventura yako katika hali ya hatari .
Hata hivyo maafisa wamesema wako tayari kwa ajili ya vitisho vyovyote kutokana na moto huo, hasa katika maeneo ambayo tayari yameungua moto na ni makavu .
Gavana wa California Gavin Newsom Jumanne aliamuru timu za kuondoa vifusi kuwa tayari huku wasimamizi wa dharura wakitarajia Dhoruba za msimu wa baridi ambazo zinaweza kusababisha maporomoko ya matope.
Baadhi ya wakaazi wa Palisades wameamua kutosubiri wakifanya kazi ya kuondoa uchafu ulioungua barabarani.
#marekani #la #wildfires #voaswahili #santamonica #malibu #makazi #california #losangeles
12 Mar 2025
- Spain's government approved a bill on Tuesday imposing massive fines on companies that use content generated by artificial intelligence (AI) without properly labelling it as such, in a bid to curb the use of so-called "deepfakes".
12 Mar 2025
- Former Philippine President Rodrigo Duterte was arrested and taken into custody on Tuesday in Manila on an International Criminal Court warrant for the "war on drugs" that defined his term in office and which killed thousands of Filipinos.