Kongamano kuhusu ugatuzi mwaka huu kuandaliwa Homa Bay

  • | KBC Video
    40 views

    Maandalizi ya makala ya 9 ya kongamano la ugatuzi la mwaka 2025 linalotarajiwa kuandaliwa katika kaunti ya Homabay kutoka tarehe 12 hadi 15 mwezi Agosti,yameanza. Kamati ya ugatuzi inayoongozwa na gavana Mutahi Kahiga imesema kongamano hilo pia litahusisha matukio ya ushirikiano kwa lengo la kuwapa wajumbe uzoefu. Kongamano hilo la kila mwaka huthaminiwa kutokana na umuhimu wake katika kuangazia manufaa ya ugatuzi nchini Kenya na pia kama jukwaa maalum la kubadilishana maarifa ili kuimarisha utekelezwaji wa ugatuzi. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: ugatuzi ni kichocheo cha usawa, ushirikishwaji na haki ya kijamii’

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive