Kuzuiliwa kwa Besigye : Makundi ya kutetea haki yaandamana Nairobi

  • | KBC Video
    263 views

    Muungano wa makundi ya kutetea haki za binadamu, wakiongozwa na Amnesty International, tawi la Kenya, Vocal Africa na chama cha madakatari na wataalam wa meno waliandamana jijini Nairobi kudhihirisha umoja na mwanasiasa wa Uganda dkt. Kizza Besigye, ambaye yuko kuzuizini nchini Uganda ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhaini Waandamanaji hao walijumuika katika barabara ya Aga Khan Walk katikati ya jiji la Nairobi kabla ya kuelekea majengo ya bunge kuwasilisha ombi la kutaka Dkt Besigye, aachiliwe huru baada ya kukamtwa akiwa jijini Nairobi mwezi Novemba mwaka uliopita. Makundi hayo ya utetezi wa haki za raia pia yaliapa kuandamana nje ya ubalozi wa Uganda humu nchini leo alasiri ambako watawasilisha ombi la kushinikiza kuachiliwa kwake wakidai ananyanyaswa kisiasa kamba haki zake za kidemokrasia zinakiukwa. Walitoa wito kwa serikali ya Kenya na jamii ya kimataifa kuingilia kati kuishinikiza serikali ya Uganda kumwachilia Besigye.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive