M23 wakaribia zaidi kuingia Goma, huku watu zaidi waendelea kukimbia makazi yao

  • | VOA Swahili
    3,429 views
    Picha za watu waliokoseshwa makazi upande wa Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati mapigano kati ya jeshi la Congo na kikundi cha wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiwa wanakaribia mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, ukiwalazimisha watu wengi kukimbia makazi yao. Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 400,000 wamekoseshwa makazi kutokana na vita hivyo tangu mwezi Januari ulipoanza pekeyake. - AFP #M23 #DRC #Rwanda #SADC #Afrika