Maafa barabarani : Watoto-3 wafariki Kirinyaga

  • | KBC Video
    40 views

    Watu watatu walifariki papo hapo na mwingine akajeruhiwa vibaya baada ya pikipiki walioabiri kugongana na lori katika eneo laGatugura kwenye barabara ya kutoka Kutus kuelekea Kimunye katika kaunti ya Kirinyaga.Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Kirinyaga Mashariki Johnson Wachira alisema lori hilo lilikuwa likielekea mjini Kutus kutoka Kimunye wakati lilipogonga pikipiki hiyo iliyokuwa imewabeba watu wanne wa umri mdogo. Wakazi waliogutushwa na ajali hiyo walisema watoto hao walitoka kijiji cha Kairegi na ni wanafunzi wa shule ya msingi ya Kimunye. Wakazi waliitaka serikali ya kaunti na ile ya taifa kuweka matuta kwenye barabara hiyo yenye shughuli nyingi pamoja na taa za barabarani ili kupunguza ajali. Mili ya waathiriwa ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kerugoya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive