Maelfu ya watu bado wamekwama kwa vifusi Myanmar, katika Dira ya Dunia TV Jumatatu 31/03/2025

  • | BBC Swahili
    10,433 views
    Ni siku tatu sasa tangu tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 7.7 kupiga taifa la Myanmar, na sasa mashirika ya kimataifa ya misaada yameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika taifa hilo. Umoja wa Mataifa umeomba msaada wa dola milioni 8 za Kimarekani, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema kuwa hospitali zimelemewa kutokana na ongezeko la majeruhi. Pia kuna hatari ya kuzuka kwa magonjwa, na maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanahitaji chakula, maji na dawa. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw