Mafunzo ya Teknolojia

  • | Citizen TV
    81 views

    Watu wanaoishi na changamoto za ulemavu katika kaunti ya Busia wamehusishwa katika mafunzo ya kujipatia mapato kupitia teknolojia ili kupunguza umasikini na ukosefu wa chakula Busia.Kwenye mpango huo wa ushirikiano baina ya taifa la uingereza na serikali ya kaunti ya Busia, watu 700 wanaoishi na changamoto hizo wamepata mafunzo na sasa wana uwezo wa kuendeleza biashara mtandaoni.