Masomo kwa wote : Shule ya wanafunzi maalum ya Apegei yahitaji msaada

  • | KBC Video
    10 views

    bodi ya usimamizi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Apegei iliyoko eneo bunge la Teso kusini kaunti ya Busia sasa inawataka wahisani kusaidia kukarabati shule hiyo ili kuwapa wanafunzi mazingira thabiti ya masomo. Mwenyekiti wa chama cha wazazi katika shule hiyo Laurence Ekasiba amesema shule hiyo ina upungufu wa madarasa, mabweni pamoja na maji safi ya kunywa. Ameongeza kuwa ukosefu wa bwalo umelazimisha wanafunzi hao kula chini ya mti. Shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 250 wenye mahitaji maalum.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive