Mkutano wa dharura Garissa kufuatika kukithiri kwa visa vya uhalifu.

  • | Citizen TV
    108 views

    Maafisa wakuu wa usalama katika eneo la Garissa wameandaa mkutano wa dharura kufuatika kukithiri kwa visa vya uhalifu katika eneo la Jarirot viungani mwa mji huo wa Garissa.

    Katika mkutano uliowahuhisha viongozi wa kijamii na wakuu wa usalama, ilibainika kuwa matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana yamechangia kuongezeka kwa visa vya uporaji wa mali na kudorora kwa hali ya usalama. Aidha, wenyeji walitahadharishwa dhidi ya kuwaficha wahalifu miongoni mwao wakionywa kuwa wao pia watachukuliwa hatua. Wenyeji walipendekeza kujengwa kwa kituo cha polisi eneo hilo ili kukabiliana na utovu wa usalama.