Mwanamke Bomba

  • | Citizen TV
    425 views

    Unapohitaji huduma za kubebewa mizigo katika soko la wakulima hapa Nairobi, jina la Leah wanjiru halitakosekana. Ni kazi ambayo haikuwa vigumu Kwake kuizamia kwani tangu utotoni amekuwa katika soko hilo ambako Mamake Mzazi anafanyia biashara. Na kama kazi nyingine,Changamoto za hapa na pale hazikosekani lakini wanjiru anajikakamua ili kukidhi mahitaji yake na ya wanawe huku akitumai kwamba siku moja atapata Ajira nyingine ambayo haina Changamoto nyingi. Leah Wanjiru anatupambia makala ya mwanamke bomba hii leo.