"Ninaweza kukufanya milionea."

  • | BBC Swahili
    953 views
    Mawakala wa ajira wanaowalaghai raia wa kigeni wanaoomba kazi katika sekta ya afya ya Uingereza wamefichuliwa kupitia uchunguzi wa siri wa BBC. BBCAfricaEye imefuatilia kwa siri mawakala wadanganyifu wa masuala ya uhamiaji wanaochukua maelfu ya pauni kutoka kwa wahamiaji wanaotamani kupata kazi Uingereza. Na kubaini mbinu za mawakala hawa, ikiwa ni pamoja na kuuza nafasi za kazi katika makampuni ya afya ya Uingereza kinyume cha sheria. Wizara ya Mambo ya ndani ya Uingereza imekiri kuwa mfumo huu unakabiliwa na udanganyifu, lakini uchunguzi wetu umeonyesha jinsi mawakala hawa wanavyoweza kuwalaghai watu kwa urahisi, kuepuka kugundulika na kuendelea kunufaika kifedha. Tazama video hii kwa urefu hapa hapa Youtube ya bbcswahili #bbcswahili #uingereza #uhamiaji Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw