Polisi Mombasa wamewakamata washukiwa 8 wa ujambazi ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakazi

  • | Citizen TV
    998 views

    Washukiwa hao walinaswa wakiwa wamejihami kwa mapanga na sururu yamekuwa wakitumia kuvunja nyumba za watu na kuwakatakata wakaazi. Genge hilo linahusishwa na visa mbalimbali vya ujambazi na kuwaibia watu, huku Kamanda wa polisi Peter Kimani akisema kuwa polisi walilalzimika kuwafuata waliotoroka hadi kilifi na kufichua maficho yao. Kimani amesema kuwa msako unaendelea na kuwa uchunguzi wa simu zilizonaswa umeanzishwa ili kukomesha kabisa mtandao wa uhalifu wa genge hilo na kuwanasa washukiwa zaidi.