Rais Ruto na Museveni wahudhuria tamasha ya Piny Luo

  • | KBC Video
    836 views

    Rais William Ruto na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni waliungana na mwaniaji wa wadhifa wa uenyekiti wa tume ya muungano Afrika Raila Odinga katika kaunti ya Siaya wakati wa siku ya mwisho ya tamasha ya kitamaduni ya Luo Piny. Marais hao wawili walikariri kujitolea kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi miongoni mwa mataifa ya Afrika kwa ajili ya maendeleo. Rais Ruto pia alizindua miradi ya maendeleo iliyogharimu serikali shilingi milioni-500 katika gatuzi la Siaya ,ukiwemo msaada wa shilingi milioni-100 kwa jamii ya wavuvi zinazoishi eneo hilo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive