Trump aanzisha rasmi sera ya jinsia mbili; kiongozi wa kanisa amuomba awe na huruma

  • | VOA Swahili
    99 views
    Rais Donald Trump ameanza utawala wake mpya wiki hii kwa kusaini mamia ya amri za kiutendaji kwa masuala mbali mbali kuanzia nishati hadi uhamiaji. Baadhi ya amri zake ni pamoja na kufuta programu za mchanganyiko, uwiano na ushiriki na kutangaza kuwa serikali ya Marekani itatambua jinsia mbili tu – mwanamme na mwanamke. “Kuanzia hivi leo, na kuendelea itakuwa ni sera rasmi ya serikali ya Marekani kuwa kuna jinsia mbili tu, mwanamme na mwanamke,” Trump alisema katika hotuba yake baada ya kuapishwa siku ya Jumatatu. Siku moja baada ya kutangaza kuwa kutakuwa na jinsia mbili tu nchini Marekani na kusaini amri za kiutendaji ili kuwakamata wahamiaji haramu, Mchungaji wa Kanisa la Episcopal Mariann Edgar Budde alimrai Trump kuonyesha huruma kwa watu ambao walikuwa na hofu ya “kile” kitakacho tokea. #trump #amriyakiutendaji #jinsia #reels #voa #voaswahili