Uongozi mpya wa CHADEMA waagizwa kuunda haraka Tume ya Ukweli na Upatanishi

  • | VOA Swahili
    40 views
    Mwenyekiti Mstaafu Freeman Mbowe ameutaka uongozi huo mpya kuunda tume ya ukweli na upatanishi ili kurudisha umoja ndani ya chama hicho uliopotea wakati wa kampeni za uchaguzi. Wakili Tundu Lissu ameshinda nafasi ya Mwenyekiti kwa kupata Kura 513, sawa na asilimia 51.5, akimshinda aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambaye amepata kura 482, sawa na asilimia 48.3, huku Odero Charlse akipata kura 1 sawa na asilimia 0.1. Hata hivyo mwenyekiti huyo Mpya Wakili Tundu Lisu amesema uchaguzi ulikuwa huru na kuvitaka vyama vyengine vya upinzani na chama tawala kuiga mfano kutoka kwao. Ripoti ya mwandishi wa VOA, Amri Ramadhani.⁣ #uchaguzi #chadema #mwenyekiti #makamu #tundulissu #freemanmbowe #voa #voaswahili