Vijana waliojeruhiwa kwenye maandamano ya Gen Z mwezi Juni-Agosti bado wanatafuta haki

  • | Citizen TV
    1,467 views

    Baadhi ya majeruhi wa maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z bado wanatafuta haki miezi sita baadaye. Daniel mwaura aliyepigwa risasi tumboni katika eneo la mlolongo ni mmoja wa waathiriwa ambao wamesalia na maumivu makali na maisha yao kubadilika kabisa baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi. Francis ode anasimulia masaibu yake huku familia ikishinikiza kukamatwa kwa wahusika.