Vita dhidi ya ufisadi kuendelezwa katika kila idara

  • | K24 Video
    17 views

    Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei ametoa onyo kwa wafanyikazi wa umma watakaozembea kazini kwamba serikali haitasita kuwafuta kazi. Koskei aliyefanya kikao na wakuu wa idara mbali mbali na mashirika ya serikali jijini Nairobi mapema leo pia amekariri kujitolea kwa rais William Ruto kuhakikisha ufisadi unakabiliwa vilivyo. Koskei pia amewaamrisha maafisa wa serikali ambao hawajachukua likizo wafanye hivyo mara moja kwani baadhi wanakwepa kupumzika ili kuendeleza ufisadi.