Waporaji na wahuni washiriki maandamano

  • | K24 Video
    54 views

    Maandamano katikati mwa jiji la Nairobi yalionekana kupoteza mwelekeo na kuonekana kuwa kitegauchumi kwa wahalifu. Baadhi ya waporaji wlaijidai kuwa waandamanaji walivamia maduka na kupora bidhaa tofauti. licha ya mahakama ya malindi kupiga marufuku ya muda utumizi wa vitoa machozi na risasi za mpira kutawanya waandamanaji maafisa wa polisi iliwabidi kuvitumia kutuliza hali, na wizi ulipozidi wafanyibiashara walijipanga kwa marungu kulinda maduka yao waliyofunga kuzuia uhalifu kuendelea. Sokomoko ilizidi kufuatia waandamanaji kufunga barabara kwa kutumia majeneza .