Wazazi wahakikishiwa mpito wa gredi-9 bila hitilafu

  • | KBC Video
    125 views

    Katibu wa elimu ya msingi Dk. Belio Kipsang amewakikishia wazazi mpito wa wanafunzi wa gredi ya tisa bila matatizo wakati shule zitakapofunguliwa tarehe 6 mwezi huu. Akizungumza mjini Mombasa wakati wa uzinduzi wa madarasa ya gredi ya tisa, Kipsang alisema madarasa 13,200 ya gredi ya tisa tayari yamejengwa kote nchini na mengine zaidi ya 2,800 yako katika viwango mbalimbali vya ujenzi.Vitabu milioni 9.9 vya gredi ya tisa vimechapishwa huku asilimia 85 za shule zikiwa tayari zimepokea vitabu hivyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive