Mchele usiofaa wapiganiwa katika eneo la Kipkenyo Eldoret

  • | K24 Video
    162 views

    Afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa katika eneo la Kipkenyo Eldoret wakati vijana waliokuwa na mawe walipovamia na kuvuruga shughuli ya kuharibu mchele usiofaa kwa matumizi ya binadamu. Shughuli hiyo ilikuwa ikiendeshwa na maafisa wa shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini. Maafisa wa KBS wakiandamana na kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu walifika katika eneo la kutupa taka mtaani huruma kabla ya vijana waliotaka mchele huo kufika na kuanza kurusha mawe. Baadhi yao walifanikiwa kuchukua magunia kadhaa.