Wamarekani 2 washukiwa wa jaribio la mapinduzi wakamatwa DRC

  • | VOA Swahili
    41 views
    Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanasema kuwa yamezima jaribio la mapinduzi mapema Jumapili na kuwakamata wahalifu, wakiwemo raia wa kigeni kadhaa. Hii ilifuatia mashambulizi yaliyofanywa katika kasri ya rais na makazi ya mshirika wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi ambapo watu watatu waliuawa katika mji mkuu, Kinshasa. Sita kati ya hao waliouawa ni pamoja na washambuliaji watatu na kiongozi wao, kiongozi wa upinzani aliyekuwa anaishi ughaibuni Christian Malanga, msemaji wa jeshi la Congo Brigedia Jenerali Sylvain Ekenge aliwaambia waandishi wa habari Jumapili usiku, akiongeza kuwa wahalifu takriban 50 walikamatwa. Video hiyo inaonyesha watu kadhaa wa Congo ambao hakutambulishwa, wanaoshukiwa kuhusika katika kile jeshi la ulinzi ilichosema kilikuwa ni mapinduzi yaliyofeli, wakiwa wamezingirwa na wanajeshi wa Congo. Wamarekani wawili, wanaoshukiwa kuhusika katika kile jeshi ilichosema ni mapinduzi yaliyofeli, wakiwa chini wamezungukwa na wanajeshi wa Congo (mtoto raia wa Marekani wa Christian Malanga katika picha ya chini, iliyozungushiwa duara jekundu). #mapinduzi #drc #jeshi #wanamgambo #felixtshisekedi #voa #voaswahili #christianmalanga #jenerali #sylvainekenge #congo #rais #felixtshisekedi