Rais Ruto asema atawabadilisha polisi wanaolinda Haiti kuwa maafisa wa kudumu wa umoja wa mataifa

  • | K24 Video
    44 views

    Rais William Ruto sasa anasema yuko tayari kuwabadilisha polisi wa Kenya wanaoendesha shughuli zao za kulinda doria Haiti hadi kuwa maafisa kudumu wa umoja wa mataifa wa kulinda amani. Rais Ruto ambaye anazuru haiti kabla ya hotuba yake ya mkutano mkuu wa umoja wa mataifa ametoa ahadi ya kuongeza maafisa 600 zaidi wa polisi kupiga jeki kikosi cha maafisa 400 walitangulia na kufikisah idadi kuwa 1000 kama ilivyoratibiwa. Rais Ruto amepongeza utendakazi wa kikosi cha kenya licha ya ghasia ambazo bado inaendelea katika taifa la haiti huku hofu kwamba magenge yanalenga maeneo mapya, na kusababisha kuhama kwa watu kuibuka.