Dr Isaac Kalua akosoa usimamizi wa shirika la KFS

  • | KBC Video
    11 views

    Kiongozi wa chama cha Green Thinking Action Dr Isaac Kalua Green ambaye pia ni mtetezi mkuu wa utunzi wa mazingira ametoa wito wa kufanyia mabadiliko usimamizi wa shirika la kuhifadhi misitu. Dr Kalua amesema usimamizi wa shirika la KFS umefeli kulinda misitu ya humu nchini na badala yake kujihusiha katika uuzaji wa miti ya kiasili ili kujipatia fedha. Kwa mujibu wa Dr Kalua, wito wa rais wa kuimarisha utandu wa misitu humu nchini huenda usitimizwe iwapo wasimamizi wa shirika hilo watasalia mamlakani.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News