Familia tatu jijini Nairobi na Mombasa zawasaka jamaa wao waliopotea kwa njia tatanishi

  • | Citizen TV
    5,394 views

    Familia tatu hapa Jijini Nairobi na Mombasa zimesalia kwenye njiapanda zikiwatafuta jamaa zao waliotoweka katika njia tatanishi. Katika mtaa wa South C, Familia ya Idd Rashid aliyetoweka tangu juma lililopita inasema imemtafuta kijana huyo bila mafanikio huku familia nyingine pia ikimtafuta kijana wao wa miaka 23. Na kama Gilbert Rono familia nyingine mjini Mombasa pia inamtafuta mfanyabiashara wa miaka 33 Yusuf Ali Abdi ambaye pia alitoweka juma lililopita