Gavana Hillary Barchok alakiwa kwa shangwe na nderemo aliporejea katika kaunti ya Bomet

  • | K24 Video
    59 views

    Gavana wa Bomet profesa Hillary Barchok alilakiwa kwa shangwe na nderemo aliporejea katika kaunti hiyo baada ya kurekodi taarifa katika afisi za tume ya maadili na kupambana na ufisadi za kanda ya kusini mwa bonde la ufa, kaunti ya Nakuru. Gavana huyo alikaribishwa na mamia ya wafuasi wake waliomsindikiza kutoka kwa makazi yake kuelekea mjini Bomet.