Goma DRC: M23 wasitisha vita

  • | BBC Swahili
    9,067 views
    Kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda limetengaza kwamba limesitisha vita mashariki mwa DRC kwa misingi ya kibinadamu. Hali ya kibinadamu imekuwa mbaya tangu mji wa Goma kutekwa na kundi la M23 wiki iliyopita. Zaidi ya watu 700 wameuawa katika mapigano huku wengine 3,000 wakijeruhiwa. Hali hii imeifanya umoja wa mataifa kutoa wito wa kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa Goma kwa ajili ya kushughulikia idadi kubwa ya majeruhi wanaohitaji huduma za matibabu katika vituo vya afya ambavyo hadi sasa vina wagonjwa wengi.