Idadi ya waliofariki kufikia leo ni 198

  • | Citizen TV
    618 views

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko kufikia leo ni 198. Idadi hii inajumuisha watu 71 waliofariki katika eneo la Mai mahiu Hapo jana. Maiti nne zaidi ziliopolewa katika aneo la Madogo kaunti ya Tana River. watu wanne wakiaga dunia katika eneo la Sindo huku wengine wakiaga dunia Homa Bay. Kufikia sasa watu 102 wamejeruhiwa katika maeneo tofauti nchini. Watu 91 hawajulikani waliko, wengi wao wakiwa katika eneo hilo la Mai Mahiu. Nyumba zilizosombwa ni 30,099 Huku Watu walioathirika kutokana na janga hili wakiwa 190,942. Kituo cha kutoa maelezo kimewekwa katika eneo la Mai Mahiu. Maafisa wa serikali kuu, ile ya kaunti ya Nakuru na Shirika la Msalaba Mwekundu wanasimamia kituo hicho.