Kindiki: Tutalipa madeni ya hospitali ya NHIF

  • | K24 Video
    19 views

    Naibu rais Kithure Kindiki amezitaka hospitali zinazongojea malipo kuwa na subira huku serikali ikishughulikia changamoto zilizopo katika mpango wa bima ya afya ya umma, SHIF, na NHIF iliyovunjwa. Akizungumza wakati wa kukagua shughuli za taifa care katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta, naibu rais amewahimiza wakenya kujiandikisha kwa taifa care chini ya mamlaka ya afya ya kijamii, SHA.