Mchambuzi Ahmed Rajab aaga dunia

  • | BBC Swahili
    2,801 views
    Mtangazaji wa zamani wa BBC, bwana Ahmed Rajab amefariki dunia leo alasiri huko London, Uingereza. Ahmed Rajab alijiunga na BBC mwazoni mwa miaka ya 1960. Baada ya kustaafu Ahmed Rajab alikuwa mmoja wa wachambuzi wa kutegemewa wa masuala ya kimataifa wa BBC hadi siku chache ziliopita. Taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa baadaye na familia yake, zikiwemo taratibu za maziko. Mara ya mwisho alifanya uchambuzi hapa katika Dira ya Dunia TV kuhusu mzozo wa Gaza Januari 15 mwaka huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.