Nairobi inaongoza kwa idadi ya wanaougua maradhi yanayotokana na ulaji wa chakula kisicho salama

  • | K24 Video
    41 views

    Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa idadi ya wanaougua maradhi yanayotokana na ulaji wa chakula kisicho salama. Wizara ya afya inasema magonjwa zaidi ya mia mbili yanaweza kusababishwa na kula chakula kisicho salama. Tume inayobuni viwango bora vya chakula, codex , inasema ulimwenguni, asilimia sitini ya wanaougua magonjwa hayo ni watu wazima, na asilimia arobaini ni watoto. Tume hiyo imeitaka serikali ya Kenya kuwekeza katika afya ya umma ili kuhakikisha uzalishaji wa chakula salama.