Serikali yatakiwa kutoa ufadhili wa shilingi bilioni 1.2 ili kuepuka uhaba wa chanjo

  • | KBC Video
    75 views

    Huenda taifa likashuhudia uhaba mkubwa wa chanjo kufikia mwezi juni mwaka huu, iwapo serikali haitatimiza wajibu wake wa ufadhili, hatua ambayo itaathiri pakubwa afya ya mamilioni ya watoto humu nchini. Chama cha wabunge wa kike KEWOPA, shirikisho la mashirika yasiyo ya kiserikali ya afya, HENNET, na wadau wengine, wameelezea wasiwasi kuhusu hatua ya serikali ya kuchelewesha malipo ya shilingi bilioni 1.2 zinazohitajika, chini ya mkataba wa makubaliano na muungano wa kimataifa wa chanjo 'Gavi' kwa ununuzi wa chanjo zinazohitajika humu nchini. Sasa wameitaka wizara za afya na fedha kuchukua hatua za dharura kutekeleza wajibu huo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive