Tisho la ndovu : Wakazi wa kijiji cha Ngari wahofia kushambuliwa

  • | KBC Video
    16 views

    Wakazi wa kijiji cha Ngari kilichoko katika kaunti ya Samburu wanakabiliwa na tisho la uvamizi wa wanyama pori hususan ndovu kutoka msitu wa Kirisia. Kwa siku kadha zilizopita, ndovu watatu wameonekana wakizurura kwenye kijiji hicho kilichoko mwendo wa kilomita saba kutoka mji wa Maralal, hali ambayo imesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wakazi. Wakazi hao sasa wanalazimika kukesha macho usiku kucha kulinda nyumba zao. Wanaitaka serikali kupitia shirika la huduma kwa wanyama pori kuchukua hatua za dharura kuepusha maafa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive