Waathiriwa wa utapeli wa sarafu waelezea jinsi walivyolaghaiwa na Springmark Investment Eldoret

  • | Citizen TV
    618 views

    Waathiriwa zaidi wa utapeli wa sarafu mjini Eldoret wameendelea kujitokeza, wakielezea yaliyojiri kwenye mikataba yao na kampuni ya Springmark Investments. Miongoni mwa waathiriwa ni William Getumbe na Susan Waititu waliotufungulia mengi kuhusu mikataba hiyo ya tangu mwaka wa 2022. Na kama John Wanyama anavyoarifu, sasa inabainika kuwa mmiliki wa kampuni ya Springmark alishirikiana na kampuni nyingine kuwahadaa mamia ya wakaazi waliotarajiwa faida kubwa