Wakazi Mugirango Kusini wapinga kuachiliwa kwa mshukiwa wa mauaji

  • | KBC Video
    22 views

    Wakazi wa eneo la Nyachenge Mugirango Kusini kaunti ya Kisii waliandamana barabarani kulalamikia hatua ya kuwaachilia washukiwa watatu wa mauaji ya kinyama ya mlinzi wa usiku na mwanawe wakati wa wizi kwenye baa moja ya eneo hilo. Washukiwa hao walikamatwa na makachero katika eneo la Gucha Kusini kuhusiana na shambulizi lililosababisha vifo vya John Otondi wa umri wa miaka 65 na mwanawe Samuel Nyamatari wa mri wa miaka 19 mnamo tarehe 26 mwezi Novemba mwaka jana. Baadaye waliachiliwa kwa misingi ya ukosefu wa ushahidi wa kutosha. Wakazi hao wameahidi kuendelea na maandamano yao hadi marehemu na familia yake watakapopata haki.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive